Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni Januari 30, 2024 limejadili na kupitisha makadirio ya bajeti kwa mwaka 2024/2025 ya Shilingi 149,456, 590,400.00
Kati ya bajeti hiyo shilingi bilioni 75,256,436,400 ni Ruzuku kutoka Serikali Kuu na Shilingi bilioni 74,200,154,000 zitatokana na mapato ya ndani ambayo ni ongezeko la asilimia nane kutoka bajeti ya mwaka 2023/2024 kwa Shilingi 11,268,407,000.00
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Songoro Mnyonge, alipongeza jitihada za Manispaa za ukusanyaji mapato, akibainisha kuwa hii imeisaidia Manispaa kupunguza utegemezi mkubwa kwa ruzuku.
Aidha, Mstahiki Meya Songoro alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kuwaletea wananchi maendeleo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.