NI KUFUATIA MPANGO WA UTOAJI WA VITAMBULISHO KWA WAMACHINGA UTAKAOWARAHISISHIA UFANYAJI KAZI ZAO BILA BUGUDHA.
Baraza la Madiwani Manispaa ya Kinondoni chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni diwani wa kata ya Msasani Mhe. Benjamini Sitta, leo limempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dr.John Pombe Joseph Magufuli, kwa mpango wake mzuri, madhubuti na wezeshi wa kuwapatia vitambulisho wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama wamachinga vitakavyowasaidia katika shughuli zao.
Akitoa pongezi hizo kwa niaba ya Baraza hilo, Meya Sitta amesema, mpango huo mkakati wa vitambulisho ni mpango ulio rahisi, rafiki, na wezeshi utakaowawezesha wamachinga kufanya kazi zao mahali popote nchi hii bila kubughudhiwa alimradi wasivunje sheria.
Ameongeza kuwa vitambulisho hivyo pia vitawasaidia si tu mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kufanya kazi zao,bali pia kwa wamachinga kutambulika kuthaminiwa na kusajiliwa katika mfumo unaojulikana.
Akiainisha viambatishi rejea ili kupata kitambulisho hicho, katibu wa kikao hicho cha baraza, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg Aron Kagurumjuli amesema, kwa wale waliosajiliwa awali kwa kinondoni wanachotakiwa kufanya ni kurejesha kitambulisho cha awali, picha moja ya passportsize, kujaza fomu yenye taarifa zako, na kiasi cha fedha shilingi elfu ishirini tu.
Katika hatua nyingine, Meya Sitta amewataka wamachinga wa Manispaa ya kinondoni kutokutumia vibaya vitambulisho hivyo kwani atakayebainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.