Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Dar es Salaam Komrade Ally Bananga, ameipongeza Wilaya ya Kinondoni katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapainduzi kwa muda wa miaka mitatu mfululizo.
Komrade Bananga ameyasema hayo wakati wa utambulisho kwa wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya uliyofanyika leo katika ukumbi wa Travetime, Wilaya ya Kinondoni.
"Nawapongeza kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya Chama kwa muda wa miaka mitatu mfululizo. Mnazidi kuifanya Kinondoni kuwa Dar es Salaam".
Aliuomba uongozi wa Wilaya na Manispaa ya Kinondoni chini ya Mheshimiwa Saad Mtambule, Mkurugenzi wa Manispaa, Bi. Hanifa Suleiman Hamza na Meya wa Manispaa, Mheshimiwa Songoro Mnyonge kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo.
Aidha, alieleza kuwa CCM na Serikali ni kitu kimoja na wanapaswa kufanya kazi kwa pamoja. "Sisi na ninyi ni kitu kimoja, hatuna sababu ya kupishana, watendaji mfahamu kuwa asiwepo yeyote wa kutukwamisha", alisema.
Kadhalika, aliwaomba Waheshimiwa Madiwani kuendelea kutimiza wajibu wao wakati wakielekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024.
Mkutano wa Halmashauri Kuu Wilaya ya Kinondoni pamoja na mambo mengine umepokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM. Awali, Kamati ya Siasa ya Wilaya ilitembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Manispaa ya Kinondoni.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:
Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.