NI BAADA YA KUZURU BANDA LA MANISPAA YA KINONDONI NA KUJIONEA SEKTA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI WALIVYOJIPANGA KATIKA KUFIKISHA UJUMBE KWA VITENDO.
Makamu wa pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Alli Idd, ameoneshwa kuridhishwa na utekelezaji wa kauli mbiu ya mwaka 2018, ya maonesho ya 25, ya nane nane Mkoani Morogoro isemayo "Wekeza katika kilimo, mifugo, na uvuvi kwa maendeleo ya viwanda "alipozuru katika banda la Manispaa ya Kinondoni lililoko katika viwanja vya Tungi Mkoani hapo.
Hali hiyo imejidhihirisha pale alipotaka maelezo kwa kina kuhusiana na utengenezaji wa Chakula cha kuku, utengenezaji wa viatu vya ngozi utokanao na ngozi za wanyama, pamoja na ufugaji wa mbuzi wa maziwa aina ya Saanen, ambao maziwa yao ni dawa inayotibu magonjwa mablimbali, na kuoanisha shughuli zote hizo na mnyororo wa thamani uliopo katika kutekeleza kauli mbiu ya mwaka huu ya maonesho ya Nane nane, hasa ikizingatiwa Sera ya Serikali ya Nchini Tanzania , chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. John Pombe Magufuli ni ya uchumi wa kati wa viwanda, kupitia malighafi zinazozalishwa na wajasiriamali wetu.
Katika ziara yake hiyo aliyoambatana na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali Balozi Seif amepatiwa maelezo ya kitaalam kutoka kwa wataalam wa sekta ya Kilimo, mifugo na uvuvi, na piá fursa ya kuzitembelea sekta hizo kwa lengo la kujionea kwa vitendo, aina ya Kilimo kitumiacho vipando vya mboga mbalimbali, kwa kutumia eneo dogo na kupata mazao mengi yenye faida, mifugo inayofugwa kitaalamu pamoja na uvuvi unaozingatia sheria na kanuni.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.