Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni, le katika Kikao Maalum limepitisha bajeti ya Shilingi za Kitanzania 135,891,778,000.00 ikiwa ni bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024.
Bajeti hiyo ina ongezeko la asilimia 8 ya bajeti ya makusanyo ya ndani ambayo kwa mwaka 2023/2024 Manispaa inatarajia kukusanya jumla ya Shilingi za Kitanzania 61,605,932,000.00. Katika mwaka wa fedha 2022/2023 mapato ya ndani ni Shilingi za Kitanzania 57,210,679,000.00 ambalo imeongezeka kwa Shilingi za Kitanzania 4,395,253,000,00.
Aidha, katika bajeti hiyo Serikali Kuu itatoa ruzuku ya Shilingi za Kitanzania 74,285,846,000.00 sawa na asilimia 55 ya bajeti nzima.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Songoro Mnyonge, akizungumza katika Baraza hilo maalum, alisema kuwa, "bajeti hii imegusa kila Kata. Bajeti hii imejielekeza vizuri katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kama tutakusanya vizuri mapato, tutaiweka sehemu nzuri Manispaa yetu."
Mstahiki Meya aliongeza kuwa kwa sasa bajeti ya Manispaa imefikiwa asilimia 45 huku Serikali Kuu ikichangia asilimia 55. " Kwa ongezeko hili la bajeti ya makusanyo ya ndani, tunazidi kuimarika na lengo ni kujitegemea.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa, Bw. Shedrack Maximilian, amelihakikishia Baraza hilo maalum kuwa Manispaa imejipanga vizuri katika ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha mwaka ujao wa fedha.
Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini: Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.