TIMU ya Wataalam kutoka Manispaa ya Kinondoni imewasili na kushuhudia maandalizi, uendeshaji na ufungaji wa michuano ya AFCON 2023 inayoendelea hapa Ivory Coast.
Timu hiyo iliyowasili Februari 9, 2024 inaongozwa na Afisa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Barbra Chiledi; inawajumuisha Afisa Uwekezaji, Bw. Shadrack Mbonika; Mchumi Bi. Mwamtum Magumbo na Afisa Habari Bw. Aquilinus Shiduki.
Pamoja na mambo mengine, timu hii ya Wataalam inaendelea kujifunza namna ya kutumia fursa mbalimbali za kiuwekezaji kupitia mashindano ya kimataifa.
Tanzania kwa kushirikiana na nchi nyingine za Afrika Mashariki inatarajia kuandaa mashindano haya mwaka 2027 ambapo kwa Manispaa ya Kinondoni inajinasibu kuwa na kiwanja chake cha mpira kilichopo Mwenge.
Kiwanja hicho kinatarajiwa kutumika katika mashindano mbalimbali ya ndani pia ya kimataifa.
Katika mechi ya kumtafuta mshindi wa Tatu, Afrika Kusini ilifanikiwa kumuondoa Congo DRC kwa mikwaju ya penati.
Fainali ya leo itamkutanisha mwenyeji Ivory Coast na mpinzani wake wa jadi Nigeria ambapo wababe hao watakutana saa mbili usiku kwa saa za Afrika Magharibi.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.