Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inatekeleza programu ya mfuko wa mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kama ilivyo kwa Halmashauri zote nchini kufuatia agizo la Serikali la mwaka 1998 kuwa Halmashauri zote nchini zianzishe mfuko huo kwa kutenga asilimia 10% ya mapato yake ya ndani.
Halmashauri imekuwa ikifuata mwongozo wa mikopo kwa kuhakikisha inaboresha mfumo huo bila kukiukwa ili kuimarisha umiliki wa fedha za mfuko wa Halmashauri.
• Kuimarisha umiliki wa fursa ya mikopo ya Manispaa.
• Kuondoa mgongano wa mikopo kati ya Manispaa na wakala.
• Kuimarisha utambulisho wa walengwa kwa kuzingatia mwongozo.
• Kuondoa gharama/udhamini wa wakala (10%) ya fedha za mikopo.
Kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018 utaratibu wa utoaji wa mikopo utakuwa kama ifuatavyo:-
Mchakato wote wa utoaji wa mikopo utasimamiwa na kuratibiwa na Halmashauri kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii, kuanzia uhamasishaji wa mikopo, kuainisha vikundi hadi hatua ya vikundi kupata mikopo yao na kufanya marejesho
• Uhamasishaji
• Uainishaji wa vikundi
• Majukumu ya wadau/viongozi
• Kujenga uwezo wa vikundi
• Ukopeshaji
• Urejeshaji
• Usimamizi na ufuatiliaji.
• Viongozi wa ngazi mbalimbali za uongozi watafanya uhamasishaji juu ya mikopo ya masharti nafuu kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
• Baada ya Uhamasishaji, wananchi wataelekezwa kwenda kwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata husika ili kuendelea na hatua zinazofuata.
• Pia utafanyika uhamasishaji wa uundaji wa vikundi na kuvijengea uwezo ili kuwa na sifa.
Baada ya uhamasishaji na uundwaji wa vikundi, zoezi litakalofuata ni kuvitambua vikundi ambavyo vitakuwa na sifa ya kukopesheka kwa kufanya yafuatayo:-
• Vikundi vya wakopaji watajiorodhesha katika ofisi zao za Kata kwa Afisa Maendeleo ya Jamii.
• Kuainisha na kuchambua vikundi vinavyostahili kupewa mikopo.
• Kutoa hati ya usajili kwa vikundi.
Katika ngazi ya Manispaa, kutakuwa na Uniti ya Mikopo ambayo itakuwa na:-
1. Afisa Maendeleo ya Jamii - Mratibu
2. Mhasibu
3. Mwanansheria
4. Mchumi.
• Viongozi katika ngazi na kada mbalimbali watafanya uhamasishaji kwa ajili ya wananchi kutambua fursa ya mikopo.
• Ofisi ya Mtaa itahusika na kuwatambulisha wakopaji na kuthibitisha ukaazi wao katika mitaa yao.
• Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kata watahusika na kupitisha majina na vikundi vinavyostahili kupatiwa mikopo.
• Afisa Maendeleo ya Jamii atahusika na uratibu wa zoezi la kuainisha vikundi vinavyostahili kupata mikopo, kujenga uwezo wa vikundi na kuviwasilisha ofisini uratibu wa mikopo.
• Umri wa mkopaji - kuanzia miaka 18.
• Wanaume iwe ni kati ya miaka 18 hadi 35
• Shughuli ambazo zitapewa kipaumbele ni pamoja na viwanda vidogo vidogo na vikundi vyenye wanachama wenye ulemavu/vikundi vya wenye ulemavu.
• Wakopaji kuwa na utambulisho wa makazi kwa kuwasilisha barua ya Mtendaji wa Mtaa anakotokea.
• Vikundi kuwa na Katiba.
• Kusaini mkataba ulioambatishwa majina ya wana kikundi ukionesha malengo ya mkopo ya kila mwana kikundi kwa kila awamu ya mkopo anaoomba.
• Kila kikundi kitalazimika kufungua Akaunti katika Benki itakayokubaliwa.
• Vikundi vitakavyokuwa na sifa ya kukopeshwa vitapatiwa mafunzo juu ya uwekaji wa akiba, kuandaa katiba, ukopaji na urejeshaji wa mikopo.
• Afisa Maendeleo ya Jamii atawasilisha taarifa ya vikundi kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata kwa ajili ya uchambuzi wa hatua ya awali.
• Kila mwanakikundi ataainisha kiasi cha mkopo anachohitaji na muda wa marejesho.
• Mikopo ya wanakikundi itajumlishwa na kupata kiasi cha mkopo wa kikundi.
• Kutokana na mahitaji ya kila mwanakikundi, itapigwa hesabu ya rejesho kwa wiki.
• Kila kikundi kitaingiziwa fedha katika akaunti katika Benki itakayokubaliwa.
• Kila mwanakikundi atarejesha kiasi cha rejesho lake kwa mkusanyaji wa fedha wa kikundi.
• Fedha zikishakusanywa, mkusanya fedha atapeleka marejesho kwenye akaunti maalum ya Manispaa.
• Mkusanya fedha atawasilisha passbook pamoja na payslip kwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata husika.
NB: Kila kikundi kitalazimika kusaini mkataba wa kumdhamini mwanakikundi mwenzao na kuhakikisha wanabeba deni la mwanakikundi mwenzao pindi anaposhindwa kulipa deni lake.
• Mfumo wa marejesho utatumika kwa kushirikiana na Maafisa wa Benki kupitia vituo vitakavyoainishwa na Kata.
• Kata itakayofanya vizuri kwa wakopaji wake kurejesha mikopo kwa zaidi ya asilimia tisini na tano (95%) itaongezewa kiwango cha fedha za mikopo.
• Kata ambazo hazitafanya vizuri hazitaongezewa fedha nyingine kwa mwaka unaofuata hadi marejesho ya fedha za awali yafikie zaidi ya asilimia tisini na tano (95%).
• Kila mwisho wa mwaka wa fedha itafanyika tathmini ya kuzitambua Kata ambazo zimefanya vizuri na zile ambazo hazikufanya vizuri.
• Taarifa ya mikopo itatolewa katika taarifa ya utekelezaji wa miradi kila robo ya mwaka katika Baraza la Madiwani.
• Kushirikiana na Benki itakayopendekezwa kwa ajili ya kurahisisha ufuatiliaji wa marejesho.
• Benki zinazopendekezwa ni TWB, NMB, CRDB, TPB, na DCB kwani Benki hizi ni za Serikali na pia zina huduma kwa ajili ya vikundi.
• Inapendekezwa kuwa mikopo itolewe mara 4 kwa mwaka (mara moja kwa kila robo ya mwaka).
• Fedha zilizokusanywa na kuchangiwa kwenye mfuko zitatolewa kwa kuzingatia uwiano kwa Kata.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.