Biashara ya vileo inatekelezwa kwa kufuata Sheria ya mwaka 1968, kifungu 28 (Liquor licence act No.28 of 1968) na marekebisho ya Sheria hiyo yaliyofanywa 2004
Maombi yote mapya ya leseni za vileo ni lazima yapitishwe na wataalam ambao wameainishwa kwenye fomu ya maombi, (Afisa Afya, Afisa Ardhi, Afisa Biashara, Polisi na Maendeleo ya Kata husika
Maombi yote yanayorudiwa (Renewal) yapitishwe na Mwenyekiti wa Kamati ya maendeleo Kata na yawasilishwe kwa Afisa Biashara anayeshughulikia leseni za vileo kwa utekelezaji.
Leseni za villeo hutolewa vipindi viwili (2) ambayo kipindi cha kwanza huanzia tarehe 01/04 hadi 31/09 na kipindi cha pili huanzia tarehe 01/10 hadi 31/03.
Maombi mapya na yanayorudishwa hulipiwa ada kama ifuatavyo: -
Aidha wanaoendesha biashara ya vileo bila kufuata taratibu zilizotajwa hapo juu huchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupelekwa Mahakamani, kulipishwa faini pamoja na adhabu "penalty" au kufungiwa biashara zao.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.