Kadi ya Msamaha wa Matibabu hutolewa kwa wazee kuanzia umri wa Miaka 60.
Mzee huyu lazima awe Mkazi wa Manispaa ya Kinondoni.
Kadi hii hutolewa bure, hakuna malipo yoyote.
UTARATIBU WA KUPATA KADI YA MSAMAHA
• Muhusika anatakiwa kupata barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa wake anakoishi.
• Barua hiyo ya utambulisho iambatishwe na picha ya passport moja.
• Baada ya kukamilisha taratibu hiyo, muhusika afike ofisi za Mganga Mkuu wa Manispaa zilizopo Mkabala na Kituo cha Afya cha Magomeni(Barabara ya Kawawa na Morogoro), kwa ajili ya kupiga picha itakayotumika kwenye kadi yake pamoja na kupewa taratibu nyingine na tarehe ya kuchukua kadi yake.
KADI YA MSAMAHA INATUMIWAJE?
Kadi hii hutumika kwenye vituo vya Afya, Zahanati pamoja na hospital zilizopo Manispaa ya Kinondoni.
Mtumiaji atatakiwa kufuata taratibu zifuatazo pindi atakapokuwa na uhitaji wa kupata matibabu.
Kwanza anatakiwa kuanzia Zahanati iliyopo karibu nae kwa ajili ya kupata huduma,itakapoonekana kunauhitaji wa uangalizi mwingine na matibabu mengine Muhusika atatakiwa kupewa barua ili aweze kwenda Kituo cha AFya kwa matibabu.
Kadi hii itatumika kwenye Hospitali ya Mwananyamala endapo tu huduma anazotakiwa kuzipata mgonjwa zimeshindikana kwenye Zahanati na vituo vya Afya na mgonjwa huyu atatakiwa kupewa barua ya kumuelekeza kwenda Hospital hiyo yaani (Referral letter) kwa ajili ya matibabu zaidi.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.