Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imezindua rasmi mpango wa huduma ya tiba kwa Kadi (TIKA) tarehe 25/07/2016. Mpango huo utatumia kadi maalumu ambayo itagharimu Tsh 40,000/=tu kwa mwaka na kukuwezesha kutibiwa mwaka mzima bila malipo ya ziada. Malipo yatafanyika ofisi ya Mganga Mkuu wa Manispaa kitengo cha fedha.
Mpango huu wa TIKA hufaidisha wanachama wasio na uwezo kupata huduma za afya zenye gharama kubwa ingawa wamelipa kidogo. Makundi mengine yatakayofaidika na mpango wa TIKA ni pamoja na wazee wasio na uwezo watoto yatima na walemavu ambao watalipiwa gharama ya kadi na Halmashauri pamoja na wadau wengine watakaojitokeza.
Mtu yeyote mkazi wa Kinondoni anahaki ya kupata Kadi.
1. Atatakiwa kuonyesha hitaji la kadi hiyo.
2. Atapewa fomu ya Kujaza, Fomu hiyo inavitu vifuatavyo:-
i. Maelezo kamili ya Muombaji
ii. Maelezo ya Usajili
iii. Uthibitisho wa Msajili.
3. Baada ya kupata fomu na kujaza, muhusika atapatiwa Invoice kwa ajili ya Malipo.
4. Malipo yote yanafanyika katika bank ya CRDB kwa Akaunti namba iliyoko kwenye Invoice.
5. Muhusika atatakiwa kupiga picha katika ofisi ya Mganga Mkuu (Picha hizo ni bure)
6. Atapewa tarehe ya kuchukua Kitambulisho.
NB: Kadi hii ya TIKA huitajika kuhuishwa kila mwaka. Malipo hayo ya Tsh 40,000/= hutumika kwa mwaka mmoja.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.