JINSI YA KUSAJILI VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI NA KUVIJENGEA UWEZO.
1. Afisa Maendeleo ya Jamii ndiye Muhusika Mkuu katika kuhakikisha vikundi vinajengewa uwezo.
2. Afisa Maendeleo ya Jamii atawapatia Mafunzo na mwongozo wa uandaaji wa Katiba.
3. Afisa Maendeleo ya Jamii atawapatia fomu ya maombi ya usajili ambayo itajazwa na viongozi.
4. Fomu hiyo itapitishwa na Afisa Mtendaji wa Mtaa kikundi kilipo.Baada ya hapo itatakiwa kupata uthibitisho wa Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata Husika.
5. Baada ya Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata kupitia Fomu na kuridhika, ataiwasilisha fomu ya maombi Ofisi ya Mendeleo ya Jamii Manispaa ambako vyeti vya Usajili vitaandaliwa na kisha Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata husika atapatiwa na kuvipatia vikundi vyake.
FOMU YA USAJILI-Maendeleo ya jamii.pdf
MUUNDO WA KATIBA-maendeleo ya jamii.pdf
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.