Kitengo cha Ushirika Manispaa ya Kinondoni kinatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria Na. 6 ya mwaka 2013 na Kanuni za mwaka 2015. Chini ya Sheria hii, Kitengo kimekuwa kikitoa mchango mkubwa katika kujenga uchumi wa wananchi wa Manispaa hii na kuwawezesha kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi kupitia Vyama vya Ushirika zikiwemo SACCOS na aina nyingine za Ushirika.
SACCOS zimesogeza huduma za kifedha karibu na wananchi na hivyo kuwezesha upatikanaji wa mikopo yenye riba na masharti nafuu iliyowezesha kuanzishwa kwa biashara/shughuli mbalimbali za kiuchumi katika Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.