Sekta ya Viwanda na Biashara hutoa ajira kwa asilimia 62 ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam. Jiji la Dar es Salaam lina jumla ya wakazi 4,364,541 kati yao watu wenye umri wa kufanya kazi (miaka 15 hadi 64) ni asilimia 66.3 (2,893,691); wengi wao wanafanya kazi za biashara na ajira viwandani.
Kuna aina tatu za biashara zinazotambuliwa
Katika Jiji la Dar es Salaam kuna bidhaa za aina mbalimbali pamoja na huduma zinazouzwa kwa kiwango kikubwa na kupelekwa nje ya Mkoa. Bidhaa hizo ni pamoja na zinazozalishwa katika viwanda viliyopo hapa Mkoani na zile zinazoagizwa toka nje ya nchi.
Hii ni biashara inayofanywa kwa kuuza bidhaa zilizonunuliwa jumla na kuuzwa kidogo kidogo kwa mlaji wa mwisho. Bidhaa hizi ni za aina nyingi sana zikiwemo vyakula, vifaa vya ujenzi, mavazi na bidhaa zingine zote za matumizi mbalimbali. Biashara hizi hupatikana katika masoko, maduka na maeneo mbalimbali yaliyotengwa kwa ajili hiyo.
Biashara hii inafanyika katika Nchi yetu na nchi za nje ambapo kuna aina: Uagizaji bidhaa toka Nchi za nje (Import) na Uuzaji bidhaa kwenda Nchi za nje (Export)
Kuna makampuni mbalimbali yanayoagiza bidhaa toka nje ya nchi na kuzisambaza mikoani. Bidhaa zinazoagiza nje ni pamoja na nguo, vifaa vya ujenzi kwa mfano mabati, magari, vipuri vya magari, vipuri vya mashine, baiskeli, pikipiki.
Bidhaa zinazouzwa nje ya nchi ni pamoja na mazao ya kilimo kwa mfano kahawa, katani, tumbaku, majani ya chai, korosho, karanga na maua. Uagizaji wa bidhaa na uuzaji wa bidhaa nchi za nje unasimamiwa na Taasisi ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tanzania Trade Development Authority (TANTRADE).
Kuna maduka makubwa yanayouza bidhaa jumla na rejareja na kuagiza bidhaa toka nje. Maduka hayo ni:-
Katika Jiji la Dar es Salaam idadi ya watu imekuwa ikiongezeka kwa haraka kutokana na vivutio vya shughuli za biashara na viwanda. Wakazi hawa hupata mahitaji yao kwa kuuza na kununua bidhaa mbalimbali kutoka kwenye Masoko. Kuna jumla ya masoko 61 yanayosimamiwa na Halmashauri za Manispaa na moja linasimamiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Kati ya Masoko ambayo idadi yake imeoneshwa hapo juu, masoko makubwa ni Kariakoo, Tegeta, Magomeni, Mwananyamala Bwawani, Buguruni, Temeke Sterio, Kawe, Ilala, Tazara (Veteririnary) na Feri. Serikali imejenga soko kubwa (Machinga Complex) linaloweza kuchukua wafanyabiashara/wajasiriamali 6,000 lakini jengo hili halijatumika/halijachukua wajasiriamali wengi kama ilivyotarajiwa.
Kuna huduma za biashara zinazotolewa na Taasisi mbalimbali.
Kuna Benki za Biashara zipatazo 34 kati ya hizo ni:
Kuna taasisi zinazotoa huduma za fedha katika Jiji la Dar es Salaam zikiwa ni pamoja na zifuatazo:-
Maduka hayo huuza fedha za ndani na za kigeni. Maduka hayo ni mengi na yamesambaa katika maeneo mengi ya Jiji.
Majengo pacha ya Benki Kuu ya Tanzania
Kuna maduka makubwa ya madawa yanayotoa huduma ya kuuza madawa kwa jumla na rejareja.
Sekta ya viwanda ni sehemu muhimu katika uchumi wa Taifa. Mkoa wa Dar es Salaam una viwanda vingi vya aina mbalimbali kufuatana na bidhaa zinazozalishwa.
Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Kuendeleza Viwanda Vidogo (SIDO) linatoa mafunzo kwa wajasiriamali na kuanzisha viwanda vidogo vidogo kama vile:-
Hii ni Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji bidhaa kwa ajili ya mauzo ya Nje. Inashughulikia maeneo yaliyotolewa na kuendelezwa kwa ajili ya kuvutia na kutoa fursa kwa wawekezaji wa ndani na nje. Maeneo haya huzalisha bidhaa kwa ajili ya kuuza nje tu (exports). Maeneo ya EPZA kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni:
Mkoa wa Dar es Salaam una vitega uchumi vikubwa vya aina ya pekee kwa ukubwa na huongeza mapato Kitaifa. Vitege uchumi hivyo ni:-
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.