Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Ally Hapi amewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Watendaji wa Kata katika Manispaa hiyo kuwahudumia wananchi bila kujali itikadi za vyama vyao.
Ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akisomewa taarifa ya Maendeleo ya Kata na Mtendaji wa Kata hiyo Bi. Stella Mfinde, na kukutana na Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Ndugumbi na kufanya mazungumzo nao wakati wa ziara yake.
Akitoa ufafanuzi wa agizo hilo Hapi amesema wako baadhi ya watendaji wa Kata na Wenyeviti wa Mitaa wamelalamikiwa kuwabagua wananchi kwa itikadi zao hali inayochangia kukosa huduma muhimu za kijamii.
Hali kadhalika, Mkuu huyo wa Wilaya ya Kinondoni Mheshiwa Ally Hapi alipata nafasi ya kutembelea miradi mingine ambayo ni ujenzi wa matundu 12 ya vyoo shule ya Msingi mwalimu Nyerere, ujenzi wa nyumba ya mwalimu sekondari ya Turiani na soko la Mabatini.
Katika hatua nyingine Hapi ameahidi kutoa shilingi laki tano kwa waalimu wa Shule ya Sekondari Turiani pindi watakapoanzisha Chama chao cha kuweka na kukopa (SACCOS).
Ndugumbi ni Kata ya sita Kati ya Kata kumi za awamu ya pili katika ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kufanya mikutano ya wananchi kusikiliza kero zoa na kuzitafutia majibu.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.