Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwezi Novemba tarehe 27, 2024 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetoa mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi.
Katika mafunzo hayo yaliyotolewa Novemba 22, 2024 katika ukumbi wa Soko la Magomen Wasimammizi wamekumbushwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali katika kufanikisha zoezi zima la kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa.
Akiongea katika mafunzo hayo Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bi Hanifa Suleiman Hamza amesema ili zoezi la uchaguzi lifanikiwe vizuri lazima Msimamizi ufuate miongozo mbalimbali ya uchaguzi iliwekwa kikanuni na kisheria.
"Sheria na kanuni zimewekwa kwa lengo mahususi ili kufanikisha zoezi zima la kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa hivyo tunapaswa kuizingatia kama zinavyotutaka," alisema Bi. Hanifa.
"Ewe Mwananchi jitokeze kupiga kura tarehe 27, Novemba 2024, kwa maendeleo ya Mtaa wako na Taifa kwa ujumla"
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.