Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa, Saad Mtambule amewapongeza Wasanii wa Filamu Tanzania kwa kuitangaza Sekta ya Utalii Duniani.
Akizungumza katika Tamasha la "Shtuka boresha Afya Yako" Oktoba 2, 2024 lililoandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA), alisema, "Niwapongeze wasanii Waigizaji kwa kubeba maono ya Rais Samia ya kuitangaza Sekta ya Utalii hasa Hifadhi yetu ya Pande inayopatikana kwenye Wilaya ya Kinondoni." Tamasha Hilo limeandaliwa Kwa kushirikiana na Umojanwa Waigizaji Mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha, Mhe. Mtambule aliipongeza TAWA kwa jitihada zake katika kuboresha hifadhi ya Pande. Hifadhi hiyo ina bustani ya Wanyamapori wakiwemo Simba, Duma, Chatu, Mamba, Nyumbu, Pundamilia na vivutio vingine.
Kwa upande wake, TAWA imeushukuru Uongozi wa Wilaya ya Kinondoni Kwa ushirikiano katika Hifadhi za Pori la Pande na Kunduchi, pia imewapongeza Wasanii wa Mkoa wa Dar es Salaam kutembelea Hifadhi hiyo.
Kadhalika, wadau wameombwa kutumia mitandao ya kijamii kuhamasisha makundi mbalimbali ili yaweze kutembelea Hifadhi hiyo Ya Pande.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.