Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, amewataka wananchi kutumia nishati safi ili kujikinga na magonjwa yanayotokana na matumizi ya nishati zisizo salama.
Aliyasema hayo Oktoba 11, 2024 kwenye Uzinduzi wa Matumizi ya Nishati Safi uliofanyika katika Uwanja wa Biafra, Wilaya ya Kinondoni.
"Wengi wenu mnafikiri matumizi ya mkaa ni nafuu kuliko kutumia gesi. Lakini madhara ya matumizi ya nishati isiyo safi ni gharama zaidi kuliko kutumia nishati safi. Utakapoambiwa inahitajika milioni kumi kwa ajili ya kutibu magonjwa yaliyosababishwa na matumizi ya mkaa, gesi inakuwa nafuu kuliko mkaa."
Katika tukio hilo, wajasiriamali 200 kutoka Manispaa ya Kinondoni , wakiwemo Baba Lishe na Mama Lishe walipokea mitungi 200 ya gesi kutoka Kampuni ya Puma. Hatua hii imelenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi kama gesi ya kupikia, ambayo ni salama kwa afya na mazingira, ikilinganishwa na kuni na mkaa ambao huchangia uharibifu wa mazingira na afya.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.