Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila amewaasa wanafunzi kuwa mabalozi wa kuwahamasisha wazazi wao kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kwenda kujiandikisha katika Daftari la Makazi.
Mhe. Chalamila alitoa wito huo alipokuwa akihutubia kwenye Bonanza la Michezo lililohusisha mchezo wa Mpira wa miguu kati ya timu ya Mpira kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa dhidi ya Timu ya Shule ya Sekondari Kijitonyama.
"Sasa watoto wangu, mpira huu tuliocheza una kauli mbiu inayosema, "Kamwambie mzazi wako akajiandikishe, ili ashiriki kuwachagua viongozi wa mitaa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa."
Pia Mhe.Chalamila aliwataka Wakuu wa Wilaya zote za Dar es Salaam kuunda timu za mpira wa miguu, mpira wa mikono pamoja na riadha.
"Kwa Wakuu wa Wilaya wote wa Dar es Salaam sasa tukaunde Timu za mpira wa miguu, mpira wa mikono pamoja na riadha ambazo tutaandaa Kongamano la pamoja ambapo timu hizo zitashindana na timu kutoka Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Shule za Sekondari kadhaa ambazo zitakuwa zimeonesha moyo mkubwa wa mazoezi na timu zote zitapewa jezi na zawadi maalum."
Aidha katika mechi hiyo Timu ya Mpira ya Miguu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam imeibuka na ushindi wa magoli mawili (2) kwa moja (1) ambapo walizawadiwa Kombe la Ushindi, Jezi pamoja na kiasi cha shilingi laki tano za kitanzania (Tshs 500,000/=).
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.