Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Saad Mtambule leo Oktoba 5, 2024 amezindua Kituo cha boda boda kijulikanacho kama “Kigogo Kona Boys” kilichopo Kata ya Kigogo.
Amewataka waendesha boda boda kuimarisha ushirikiano baina yao pamoja na kuheshimu Viongozi ili kufikia malengo yao
“Endeleeni kutii sheria pasipo shuruti ikiwemo kupata mafunzo, kufuata sheria za barabarani na kutoruhusu uhalifu katika maeneo yenu”. Amesema Mhe. Mtambule.
Aidha, amewataka vijana wote kujiandikisha katika daftari la kupiga kura ambapo zoezi hili litaanza tarehe 11 Oktoba hadi 20 Oktoba 2024 ili waweze kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.