i. Kuratibu na kusimamia uwepo wa miundombinu ya msingi toshelevu shuleni ikiwa ni ujenzi/ukarabati wa vyumba vya madarasa, vyoo vya wanafunzi, nyumba za walimu, maktaba, majengo ya utawala na vituo vya walimu.
ii. Kuhamasisha na kuratibu uandikishaji wa watoto wa rika lengwa katika darasa la awali, darasa la kwanza na MEMKWA ikiwa ni pamoja na wanafunzi wenye mahitaji maalum pamoja na kusimamia mahudhurio yao kwa shule za Awali na Msingi za Serikali na zisizo za Serikali.
iii. Kuratibu matumizi sahihi ya ruzuku za uendeshaji wa shule.
iv. Kuratibu na kusimamia utoaji wa elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi kwa walioikosa katika vituo 18 vilivyosajiliwa.
v. Kufanya ufuatiliaji na kusimamia ufundishaji na ujifunzaji shuleni ili kuhakikisha ufaulu wa mtihani/upimaji wa kitaifa unaongezeka na hakuna mwanafunzi anayehitimu Elimu ya Msingi bila kumudu stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).
vi. Kuratibu na kudhibiti uwepo wa vifaa toshelevu vya kufundishia na kujifunzia shuleni hususan vitabu vya kiada vinavyosambazwa na Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA).
vii. Kuratibu zoezi la ukusanyaji na ujazaji wa takwimu za kielimu katika sensa ya elimu msingi.
viii.Kuthibitisha uhamisho wa wanafunzi wanaohama na kuhamia kutoka shule moja kwenda nyingine ndani na nje ya Manispaa.
ix. Kusajili madeni ya walimu yasiyo ya mshahara katika mfumo wa madeniMIS.
x. Kuendesha mafunzo ya mifumo ya FFARS, MadeniMIS, PReM na SiS pamoja na taratibu na kanuni za manunuzi ya umma kwa walimu wakuu wa shule za serikalii na zisizo za serikali ili kuwawezesha kutumia mifumo hiyo kwa ufanisi kwa utendaji kazi wa kila siku.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.