• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

WATANZANIA WAMEASWA KUZINGATIA FALSAFA YA 4R KATIKA KULETA MAENDELEO ENDELEVU

Tarehe iliyowekwa: December 9th, 2022

Katibu Mkuu Ofisi ya  Waziri  Sera Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu  amewaasa Watanzania kuielewa na kuizingatia falsafa ya 4R iliyoasisiwa na kutumiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa majukumu yetu ili kuyafikia mafanikio na kuwa na maendeleo endelevu.

Hayo ameyasema katika hotuba ya ufunguzi wa kongamano/mdahalo wa kilele cha maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru yaliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa Manispaa ya Kinondoni.

Akifafanua falsafa hiyo ya 4R alisema inahusu mambo manne ya msingi ya kuzingatiwa ambayo ni Maridhiano , Ustahimilivu, Mageuzi na Ujenzi mpya (Reconciliation, Resilience, Reforms and Rebuilding).

Kuhusu Maridhiano (Reconciliation) alitaka kuhimizwa umoja na amani katika Taifa kwa kuhuisha moyo wa kitaifa na kuinganisha nguvu ya pamoja katika kuleta maendeleo.

Alisisitiza umuhimu wa kuachana na migogoro na mifarakano na kutembea pamoja na kufika pamoja katika safari ya kuleta maendeleo endelevu ya Taifa letu.

Akizungumzia Ustahimilivu (Resilience) amesisitiza umuhimu wa kuzitumia changamoto kama fursa katika kuleta maendeleo kwani katika dunia ya sasa changamoto haziepukiki kwani ni dunia ya sayansi na teknolojia na lazima tukabiliane na kila changamoto kwa Ustahimilivu.

Kuhusu Mabadiliko (Reforms) aliwataka Watanzania kutokuwa watumwa wa historia na lazima kuwa tayari kwa mabadiliko pale yanapohitajika ili kuyafanya mambo kwenda mbele. 

Pia aliwataka Watanzania kuwa tayari kujifunza kutoka nchi na jamii nyingine zilizofanikiwa kama China, Singapore na Thailand.

Akizungumzia dhana ya Ujenzi mpya (Rebuilding) alisisitiza umuhimu wa kujifanyia tathimini kwa kuangalia mapungufu yaliyopo na kuyafanyia kazi na kusonga mbele katika kusukuma maendeleo.

Mwisho alisisitiza kama Taifa ni muhimu kuitumia dhana ya 4R katika kusukuma maendeleo. Alisema kuwa dhana hii inaungatia historia yetu uhalisia na kutupeleka  mbele (Historic, Realistic and Futuristic) na kwamba  inaunganisha historia ya nchi yetu kwa kulinganisha na hali halisi ya  sasa ili kusonga mbele zaidi katika mafanikio.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Gondwin Gondwe alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kukubali kuwa Mgeni rasmi katika kongamano la kilele cha maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania katika Wilaya ya Kinondoni na kuelezea mafanikio ya sekta  zote yaliyofikiwa na Manispaa kwa miaka 61 ya Uhuru.

Kongamano hilo limehudhuriwa na makundi mbalimbali ya wadau wote wa Manispaa yaliyotanguliwa na shughuli mbalimbali za kijamii yaliyoambatana na  mashindano pamoja na washindi kupewa zawadi.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.