• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

WAKANDARASI WA BARABARA KOTE NCHINI WAMETAKIWA KUHAKIKISHA WANATEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA WELEDI NA KWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU KATIKA KUHAKIKISHA WANAFIKIA VIWANGO VYA UJENZI VILIVYOKUBALIWA NA KWA UBORA ULIOKUSUDIWA.

Tarehe iliyowekwa: January 10th, 2018

Wakandarasi wa barabara kote nchini wametakiwa kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa uadilifu, na kwa weledi mkubwa wakizingatia sheria, kanuni na taratibu katika kuhakikisha wanafikia viwango vya ujenzi vilivyokubaliwa  pamoja na ubora uliokusudiwa. 

 Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Alli Hapi alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea utekelezaji wa barabara zinazojengwa chini ya mradi wa DMDP, pamoja na zile zinazofanyiwa matengenezo chini ya TARURA.

 Amesema  Serikali imeamua kuelekeza nguvu kubwa katika kuhakikisha inarejesha miundombinu iliyoharibika pamoja na kujenga miundombinu mipya inayoendana na ongezeko kubwa la watu, kwa kuhakikisha inatekelezwa kwa ubora na viwango vinavyokubalika. 

 "Serikali inafanya kazi kubwa katika Wilaya ya Kinondoni kurejesha miundombinu ambayo iliharibika, iliyojengwa zamani, lakini pia kujenga miundombinu mipya, ambayo inaendana na idadi ya ongezeko la watu, na ongezeko la kiasi kikubwa cha maji kinachotokana na mvua katika misimu mbalimbali.......nitoe Rai kwa watu waliopewa dhamana ya kuhakikisha barabara, mitaro pamoja na miundombinu yote ambayo tumeitembelea inajengwa, wakiwemo wakandarasi na wahandisi, wafanye kazi kwa kuzingatia weledi, ubora na viwango vya hali ya juu, hatutamvumilia Mhandisi yeyote au Mkandarasi yoyote, atakayekwenda kutujengea barabara chini ya viwango"Amesisitiza  Hapi

 Naye Maneja wa TARURA Manispaa ya Kinondoni Bw. leopod Rungi amewaasa wananchi kutokufanya Maendeleo yeyote pembezoni mwa hifadhi ya barabara, kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na watakaobainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. 

 Katika hatua nyingine Mratibu wa DMDP Manispaa ya Kinondoni Bw. Mkelewe Tungaraza ameahidi kutekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya la kuhakikisha wanasimamia ubora wa kazi zinazoendelea za ujenzi wa barabara pamoja na kuwashughulikia wale wote waliojenga pembezoni mwa hifadhi ya barabara kinyume cha sheria kwa kuwapa Notisi ya siku Saba ya kuondoa majengo yao wenyewe. 

 Barabara alizozitembelea Mkuu huyo wa Wilaya katika ziara yake ni pamoja na barabara ya Mikumi,  Idrissa,  Chemchem, Tanesco soko la Samaki, Mazinde Viwandani ,Viongozi pamoja na Jengo la ofisi za DMDP. 

 imetolewa na
 Kitengo cha Uhusiano na Habari.
 Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.