• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

MKUTANO WA WADAU KUHUSIANA NA MASWALA YA USAFI KINONDONI WAFANYIKA LEO

Tarehe iliyowekwa: August 2nd, 2018

NI KUFUATIA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, MH PAUL MAKONDA, LA KUZITAKA KATA NA MITAA YOTE KUWA MISAFI.

Akifungua mkutano huo uliohusisha watendaji wa Kata, Mitaa pamoja na wadau wa maswala ya usafi, sheria na afya, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Dr. Patricia Henjewele amesema ni kwa lengo la kutathmini zoezi la usafi linaloendelea,  na pia kukumbushana njia za kudhibiti na kutatua changamoto zinazojitokeza, wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo, ili ufumbuzi yakinifu wenye ufanisi uweze kuleta tija kwa maslahi mapana ya wananchi wa Kinondoni.

 Amesema kukutanisha makundi haya muhimu pia kutawezesha kufikia malengo ya utekelezaji wa agizo hili ikiwa ni pamoja na kuhakikisha swala la changamoto linatatuliwa na kuweka mikakati thabiti itakayomwezesha kila mmoja kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu katika kutekeleza agizo hili la Mkuu wa Mkoa,  la kuhakikisha maeneo yote ya Kata na Mitaa yanakuwa safi.

 "Tuna kama wiki mbili tangu tuanze zoezi hili la kuhakikisha jiji letu linakuwa safi, lakini ziko changamoto ambazo tumeona zimejitokeza, hivyo tumeamua kukutana ili kukumbushana jinsi ya kudhibiti changamoto hizi ili kazi yetu iweze kuwa na ufanisi mkubwa, na pia ni kutaka kukumbushana wajibu wetu katika hili, tusijejipangia majukumu ya ziada."Amebainisha Dr Patricia.

Akifafanua taratibu na wajibu wa mtumishi katika kutekeleza majukumu yake Bi Elly Makala Afisa kutoka Takukuru amesema wajibu wa Mtumishi ni kusimamia misingi ya sheria inayomtaka kutekeleza majukumu yake kwa uwazi, weledi na bila kumuonea mtu kutakakoondoa mianya ya rushwa.

Ameongeza kuwa Utumishi wa Umma hauna hiari bali wajibu katika kutekeleza limpasalo Mtumishi kwa wakati, hivyo kwa swala la usafi kila Mtumishi wa Umma akawe balozi wa usafi kwa kuwaelimisha wananchi umuhimu wake na adhabu atakayopatiwa mara baada ya kukiuka misingi ya usafi kwenye eneo Lake.

Akiainisha mada zitakazojadiliwa kwenye mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Dr. Patricia Henjewele amesema ufundishwaji wake ni kwa lengo la kuwasaidia kujua mipaka yao ya kazi ili kutoenenda kinyume na kusudio la sheria, na kuzitaja kuwa ni mada kuhusiana na sheria zinazohusiana na maswala ya rushwa, Ufafanuzi wa sheria zinazotakiwa kutumika wakati wa kusimamia maswala ya usafi, na wajibu umpasao mtendaji wa Kata au mtaa kusimamia wakati wa utekelezaji wa majukumu ya kiserikali.

Mkutano huo uliofanyika leo katika viwanja vya Manispaa, umehudhuriwa pia na wadau kutoka Takukuru, jeshi la polisi, vijana wa jeshi la mgambo, na vijana waliohitimu mafunzo ya JKT.


Imeandaliwa na

Kitengo cha Uhusiano na habari.

Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.