• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

KOREA YA KUSINI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA MAHUSIANO KATI YAKE NA MKOA WA DAR ES SALAAM

Tarehe iliyowekwa: May 30th, 2019

NI  ULE WA MIAKA MITATU UNAOHUSU KUWAJENGEA UWEZO WATAALAM WA KILIMO KATIKA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA ZA KILIMO CHA MJINI CHA KISASA .

Korea ya Kusini jimbo la Gyeongsanam imeoneshwa kuridhishwa na utekelezaji wa makubaliano yalioingiwa kati yake na Mkoa wa Dar és salaam, yahusuyo utoaji wa huduma ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam wa kilimo, kuhusiana na teknolojia za Kilimo chá kisasa cha mjini ili kukabiliana na changamoto zilizopo kama ufinyu wa ardhi na magonjwa ya mimea.

Hayo yamedhihirika leo wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya ujumbe kutoka korea ya kusini, waliozuru kwa lengo la kufanya majadiliano ya namna ya kuingia upya mkataba mwingine, wenye lengo la kuboresha zaidi sekta hiyo ya kilimo hasa upande wa matumizi ya teknolojia ya vifaa vya kisasa kwa matumizi madogo ya ardhi yenye tija, baada ya ule wa awali kuisha.

Akipokea ujumbe huo kutoka Korea ya Kusini, ulipozuru kituo cha kilimo Malolo Kinondoni, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Mhe. Benjamin Sitta  amesema Dar es salaam hususani Kinondoni leo imefungua ukurasa mpya wa maendeleo katika sekta ya kilimo cha mjini kwani mkataba huo uliodumu kwa miaka mitatu umeibua ari mpya ya maendeleo na kuleta mapinduzi katika sekta hii kwa kuiniua pato lá mkulima pindi atumiapo utaalam huo ulio rahisi na wamatumizi madogo ya eneo.

"Hakika mapinduzi ya kilimo cha mjini yameneemeshwa vilivyo kupitia uhusiano wetu na Korea kusini maana tumejifunza mambo mengi sana kupitia wao na tunaamini hatutaishia hapa tutaenda mbele zaidi"ameeleza Msitahiki Meya.

Naye  Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji wa Mkoa Dar es salaam Dkt. Elizabeth Mshote amesema kuwa Manispaa za jiji la Dar es salaam zimenufaika vilivyo kupitia uhusiano huo na Korea kusini na kuanishia kuwa awamu ijayo itakuwa nzuri zaidi kwani ushiriki utajikita zaidi katika miundombinu ya kilimo tofauti na ule wa awali uliokuwa na lengo la kujengea uwezo wataalam hao wa kilimo.

Kwa upande wao Mr. Lee, Do Wan ambaye ni Mkurugenzi wa Division ya Ushirikiano na nchi za nje kutoka Jimbo la Gyeongsangnam na Dkt Lim Chae Shin kutoka Kituo cha mafunzo ya technologia ya kisasa ya kilimo ATEC kilichopo Mjini Jinju Korea kusini, amesema kuwa anaamini Tanzania inaweza kabisa kufikia Korea kusini maana mwitikio uliooneshwa ndani ya miaka mitatu ni wa kipekee sana na  unadhirisha hamu ya mapinduzi ya kilimo ndani ya mioyo yao.

Hafla hiyo imeshirikisha wataalamu wa sekta ya kilimo kutoka Halmashauri zote tano za mkoa wa Dar es  salaam, pamoja na KOICA.

Imeandaliwa na

Kitengo cha Habari na Uhusiano

Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.