• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Afya na Usafishaji
      • Mipangomiji na Maendeleo ya Makazi
      • Kilimo na Mifugo
      • Elimu Sekondari
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Matukio ya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo cha mijini
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Maji na Usafishaji
    • Ujasiriamali na utoaji wa mikopo
    • Ushauri katika Kilimo
    • Elimu ya ufugaji, mifugo na uvuvi
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Baraza la Madiwani
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

KINONDONI YAWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI KUPITIA MIKOPO YA 10% YA TSH. BILIONI 3.9 ROBO YA NNE YA MWAKA 2021/22

Tarehe iliyowekwa: June 27th, 2022

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imewawezesha wananchi kiuchumi kwa kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi za Kitanzania bilioni 3.9 katika mwaka robo ya nne ya mwaka (Aprili-Juni) wa fedha 2021/2022 kupitia asilimia kumi ya mapato yake ya ndani kwa jumla ya vikundi 286, ambapo kati yake vikundi 182 vikiwa ni vya wanawake, vikundi 90 vya vijana na vikundi 14 vya watu wenye ulemavu.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya hundi ya mfano mgeni rasmi Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe ameipongeza Halmashauri kwa jinsi ambavyo imeweza kufanya usimamizi na utoaji wa mikopo kwa makundi hayo maalum na kuhakikisha kwamba maagizo ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhusu utoaji mikopo bila riba yanatekelezwa na kuwafikia walengwa kwa wakati.

“Niwapongeze wanufaika wote wa mikopo ya asilimia kumi na ambao mnafanya marejesho kwa wakati”. Unaporejesha mikopo unatoa fursa kwa vikundi vingine vyenye sifa kuweza kukopa lakini pia unajijengea sifa ya kukopeshwa kwa mara nyingine. Alifafanua Gondwe.

Mkuu wa Wilaya pia ametoa ahadi ya kushirikisha taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi ikiwemo SIDO, BRELA na taasisi za kifedha kwa ajili ya kuwajengea elimu ya ujasiriamali, utafutaji masoko na uwekaji wa akiba wanufaika wa mikopo.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa, Mhe. Songoro Mnyonge amesema kuwa Halmashauri imeweza kutoa mikopo mingi kutokana na ukusanyaji mzuri wa mapato ya ndani jambo ambalo linapelekea ongezeko la fedha za mikopo na utoaji wa mikopo kwa wakati na amewaomba wananchi kuendelea kuwa wachangiaji wazuri wa mapato ya Serikali.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti baadhi ya wawakilishi wa vikundi hivyo wameipongeza Halmashauri kwa jitihada hizo na wameahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kufanya marejesho na kupata fursa ya kuweza kukopeshwa tena.

Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Manispaa ya Kinondoni imeweza kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi za Kitanzania bilioni 6 na katika mwaka wa fedha 2022/2023 Manispaa inatarajia kutoa mikopo ya jumla ya shilingi za Kitanzania bilioni 4.6 ili kuwawezesha makundi maalum kuanzisha na kuendeleza shughuli zao za ujasiriamali zitakazowawezesha kujiongezea kipato na kushiriki kikamilifu katika ukuaji wa uchumi

Rai imeendelea kutolewa kwa watu wenye ulemavu kuchangamkia fursa kukopa ambapo marekebisho ya Kanuni ya mwaka 2021 yanaruhusu idadi ya wanaojiunga kwa watu wenye ulemavu ambapo hata mlemavu mmoja anaweza kuomba na kupatiwa mkopo.

Matangazo

  • MABADILIKO YA VITUO VYA KUFANYIA MAFUNZO YA SENSA July 30, 2022
  • MABADILIKO YA SIKU YA MAFUNZO YA WASIMAMIZI WA MAUDHUI, WASIMAMIZI WA TEHAMA NA MAKARANI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 July 28, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO YA SENSA KWA MAKARANI, WASIMAMIZI WA MAUDHUI NA TEHAMA TAREHE 27 JULAI, 2022 WILAYA YA KINONDONI July 27, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA SENSA 2022 July 19, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • "AHIMIZA UADILIFU WAKATI WA SENSA" DC GONDWE KINONDONI

    July 28, 2022
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI AFYA NA ELIMU KINONDONI IMEFANYA ZIARA KATA YA KAWE

    July 28, 2022
  • ZIARA YA KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI KINONDONI YATEMBELEA KATA YA TANDALE NA ASASI YA PHSRF

    July 27, 2022
  • ZIARA YA KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI KINONDONI YATEMBELEA KATA YA TANDALE NA ASASI YA PHSRF

    July 27, 2022
  • Tazama zote

Picha Jongefu

UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • VITUO VYA KUKUSANYIA MAPATO
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • RATIBA YA MSTAHIKI MEYA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255 22 2170173

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.