• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

KINONDONI YAPULIZA DAWA HOTELI ZA KITALII KUDHIBITI CORONA

Tarehe iliyowekwa: April 3rd, 2020

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeendelea kupambana vikali kuthibiti kuenea kwa virusi vya COVID 19 (Corona) kwa kupuliza dawa katika hotel za kitalii zilizopo katika Halmashauri hiyo.

Hatua hiyo ni muendelezo wa mkakati uliowekwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongolo, Mkurugenzi Aron Kagurumjuli, Mstahiki Meya Benjamini Sitta, pamoja na Mganga mkuu Samweli Laizar kwa pamoja, katika kuhakikisha kuwa  maambukizi ya  Virus hivyo hayasambai kwa wananchi na hivyo wanaendelea kuwa salama.


Akizungumza wakati wa zoezi hilo Kaimu Mganga mkuu wa Kinondoni, Dk. Said Hemed amesema kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa salama katika kuepukana na maambukizi ya magonjwa ya mlipuko.

Amefafanua kuwa mbali na kuthibiti maambukizi ya virusi vya Corona, lakini pia wanachukua tahadhari ya mlipuko wa homa ya dengu kwakuwa hivi sasa ni kipindi cha mvua.

Ameongeza kuwa kupuliza dawa katika maeneo hayo ni mahususi kwakuwa wageni wengi hufikia katika hoteli hizo na kwamba wataendelea kuthibiti kwenye maeneo mbalimbali  ili virusi hivyo visienee kwenye makazi ya wananchi.

“ Tunapopuliza hizi dawa ni kwa malengo mawili, kwanza tunathibiti Corona isisambae lakini pia tunathibiti homa ya dengue, ukiangalia kipindi hiki ni cha msimu wa mvua, magonjwa mengi ya mlipuko hutokea , kwa hiyo hii ni njia ya kuwakinga wananchi wetu wa Kinondoni wasipate maambukizi yoyote” amesema Dokta Hemed.

Aidha ameongeza kuwa” hotel hizi za kitalii ni maarufu na ndio ambazo zinapokea wageni wengi, niwasishi sana waendelee kuchukua tahadhari kwakutoa ushirikiano na Halmashauri yetu ili mlipuko huu usiendelee kwenye maeneo watu.

Awali Kinondoni ilianza mchakato huo wa kupuliza dawa katika vituo vya daladala, mwendokasi, na maeneo yenye mikusanyiko ya watu ikiwemo Kanisani na Misikitini pamoja na maeneo ya wananchi na kwamba bado zoezi hilo linaendelea.

Hadi sasa zoezi la utoaji elimu kwa wananchi wa Kinondoni linaendelea kwani Kata 20 zilizopo kwenye Halmashauri zimeshafikiwa sambamba na matangazo ikiwemo kubandika mabango, kugawa vipeperushi kwa wananchi vyenye ujumbe wa kuelimisha namna ya kujikinga na virusi vya COVID19 ( Corona).

Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.