• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

KINONDONI YAKABIDHIWA MAKTABA YA KISASA YENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI THEMANINI KUTOKA KWA KOREA YA KUSINI.

Tarehe iliyowekwa: October 16th, 2017

 Manispaa ya Kinondoni imekabidhiwa Maktaba ya kisasa yenye thamani ya zaidi ya milioni themanini kutoka Korea ya Kusini kwa lengo la kuimarisha mfumo wa Elimu kwa shule za msingi utakaowajengea wanafunzi Utamaduni wa kusoma. 

 Maktaba hiyo  imepokelewa leo na Mstahiki Meya Manispaa Kinondoni Mh Benjamin Sitta katika tafrija iliyofanyika kwenye viwanja vya shule Msingi Bongoyo .

Akipokea maktaba hiyo Meya Sitta amesema anafurahishwa zaidi kuona tunapiga hatua katika mfumo mzima wa elimu kwa kuwa na maktaba ya kisasa inayotumia mifumo ya  kiteknolojia kitu ambacho  kitamjengea mtoto utamaduni wa kupenda kusoma. 

 "Nimefurahi Sana kwasababu library hii ni ya kisasa unaweza kuona mandhari yake ni nzuri, wameenda kiteknolojia zaidi "amesisitiza Meya. 

 Aidha amemshukuru Balozi wa Korea ya kusini kwa kuona umuhimu wa kuwekeza katika Elimu kitu ambacho kitamkuza mtoto na kumfanya kuwa na Utamaduni wa kusoma. 

 Naye Balozi wa Korea ya Kusini nchini Tanzania Ndg Keum Young Song amesema Serikali yake  itaendelea kusaidia miradi ya ujenzi wa maktaba ndogo kwa shule za Msingi ili iweze kusaidia wanafunzi kusoma vitabu vya kiada na ziada kwa lengo la kupata misingi mizuri katika elimu. 

 Akifafanua umuhimu wa maktaba kwa wanafunzi Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Kinondoni Ngd Kiduma Mageni amesema Maktaba ndio eneo pekee ambalo mwanafunzi anaweza kuwa na utulivu katika kusoma na kutafakari kwa kina bila kusumbuliwa na mtu yeyote. 

 Amesema Kinondoni inao mpango madhubuti wa kuziboresha shule zake kwa maana ya nyenzo za kufundishia pamoja na Mazingira rafiki ya kusomea yatakayomwezesha mwanafunzi kujenga utamaduni wa kujisomea na hasa ikizingatiwa maktaba hii ni ya kisasa kabisa yenye vifaa vyote vinavyohitajika kwa mwanfunzi kusoma bila malipo ya aina yeyote. 

 "Sisi Kinondoni tunataka tuoneshe mfano kwa vitendo, kwa kuunga mkono juhudi za Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania za kutoa elimu bila malipo, tunashule kumi na tano, hii ni mojawapo, ambazo tunataka ziwe za kwanza kwa kipindi cha mwaka 2015 hadi 2020, ziwe shule zaidi ya shule zisizokuwa za Kiserikali "Ameongeza Mageni

 Akizitaja changamoto za shuleni hapo, Mwalimu Mkuu wa shule ya Bongoyo Bi Alice Martine amesema shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa nyumba za waalimu, miundombinu ya maji kwenye vyoo, miundo mbinu ya umeme, na Samani za ofisi. 

 Korea Kusini imetimiza miaka ishirini na tano ya urafiki kati yake na Nchi ya Tanzania na hadi kufikia leo kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa kwetu na Balozi Keum Young Song imesema mpaka sasa imeshajenga jumla ya maktaba ndogo kumi na moja kwenye shule za msingi hapa Tanzania.

 Imetolewa na
 Kitengo cha Uhusiano.
 Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.