• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fukwe na Visiwa
    • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Matukio ya Utalii
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Meya
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Iliyopangwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Habari

DAWASCO YAPEWA SAA 24 KUPELEKA MAJI SOKO LA WAMACHINGA LA COCACOLA MWENGE

Tarehe iliyowekwa: August 18th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa Godwin Gondwe, ametoa saa 24 kwa DAWASCO kupeleka maji kwenye Soko la Wamachinga la Cocacola, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Agizo hilo amelitoa leo wakati akipokea meza 300 za wafanyabiashara ndogondogo (Wamachinga) zilizotolewa na Kampuni ya Cocacola jijini Dar es Salaam. Alisema, “Nimepokea ombi lenu, hivyo ninaagiza kuwa DAWASCO ndani ya masaa 24 kuanzia leo muwe mmepeleka maji kwenye soko hilo.”

Agizo hilo limefuatia ombi la Mwenyekiti wa wafanyabiajshara hao, Bw. Abdallah Mwakilima, aliyeomba kupatiwa huduma ya maji ili yaweze kutumika katika choo kilichojengwa na Manispaa ya Kinondoni. “Mheshimiwa Mkuu wa wilaya, tunaomba utuzindulie choo chetu ambacho Manispaa imekijenga kwa gharama ya shilingi milioni 50. Tatizo lililopo ni kuwa choo hicho hakina maji,” alisema Mwakilima.

Kampuni ya Cocacola imetoa meza bure kwa wafanyabiashara hao ikiwa ni lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita za kuwapatia mazingira mazuri wafanyabiashara hao.

Aidha Bw. Mwakilima pamoja na kutoa shukrani kwa Manispaa ya Kinondoni na kwa Kampuni ya Cocacola, pia aliomba eneo hilo kuwekewa kivuli ili kuwakinga dhidi ya jua na mvua wafanyabiashara hao.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Bi Hanifa Suleiman Hamza, aliwataka wafanyabiashara hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali na Kampuni ya Cocacola. 

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Songoro Mnyonge, alisema kuwa zoezi la kuwapatia vitendea kazi wafanyabiashara hao ni mwendelezo wa kampeni ya Safisha Pendezesha Dar es Salaam. “Wafanyabiashara mkikaa sehemu nzuri kwa kupangwa pia inasaidia kuisafisha na kuipendezesha Manispaa yetu ya Kinondoni,” alisema.



Imeandaliwa na

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • PONGEZI June 07, 2023
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI-DEREVA DARAJA II April 24, 2023
  • MABADILIKO YA SIKU YA MAFUNZO YA WASIMAMIZI WA MAUDHUI, WASIMAMIZI WA TEHAMA NA MAKARANI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 July 28, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • AFISA ELIMU MSINGI KINONDONI APONGEZWA

    May 19, 2023
  • JAPAN YAIPATIA MSAADA MZIMUNI SEKONDARI

    March 15, 2023
  • VIKUNDI VYAASWA MATUMIZI SAHIHI YA MIKOPO

    February 18, 2023
  • "HAKUNA TIMU KUBWA ZAIDI YA KMC FC"

    February 18, 2023
  • Tazama zote

Picha Jongefu

VITUO VITANO VYA MSAADA WA MFUMO WA TAUSI, KITUO CHA MIITO YA SIMU KUBORESHA UKUSANYAJI WA MAPATO
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
  • TAARIFA KWA UMMA
  • RATIBA YA MSTAHIKI MEYA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255 22 2170173

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.