• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

ALAT YAIPONGEZA MANISPAA YA KINONDONI KWA KUTEKELEZA MIRADI MIKUBWA KWA KUTUMIA FORCE ACCOUNT, YATAKA HALMASHAURI NYINGINE ZIIGE

Tarehe iliyowekwa: November 21st, 2019

Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania ( ALAT) imeipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa kutekeleza miradi  mikubwa ya kimkakati kwakutumia Local Fundi (Force Account).


Akizungumza na watendaji wa Halmashauri hiyo mara baada ya kukamilisha ziara ya kukagua miradi ya Halmashauri hiyo,  Makamu Mwenyekiti wa ALAT , Stephano Mhapa amesema kuwa Mkurugenzi Mtendaji Aron Kagurumjuli na timu yake wamefanikisha kujenga miradi mikubwa ya maendeleo kwa kutumia mafundi wa kawaida jambo ambalo limeonyesha  nizamu ya matumizi mazuri ya fedha za serikali.


Amefafanua kuwa mradi wa Zahanati ya Mikoroshini iliyopo Kata ya Msasani imejengwa kwa shilingi milioni 400.8 kwa kutumia mafundi wa kawaida wakati kwa mkandarasi wakutangaza tenda ingetumia milioni 700 na kwamba Halmashauri hiyo imeokoa kiasi cha shilingi milioni 300.


Aidha Mhapa amesema kuwa“ ukiangalia Zahanati hii imekamilika vizuri na imara , tumejionea wenyewe, Mkurugenzi na timu yako tunakupongeza sana, na halmashauri nyingine ziige mfano huu kutoka kwako, kazi ni kubwa uliyoifanya lakini gharama yake ni ndogo, haya ni matumizi mazuri ya fedha za serikali.”


Akizungumzia mradi wa Soko la kisasa la Magomeni, linalojengwa kwa shilingi zaidi ya bilioni 8.9 na Kituo  cha Afya kilichopo Kigogo kinachojengwa kwa shilingi milioni 700 , Mhapa amesisitiza kuwa Halmashauri ya Kinondoni inapaswa kuigwa na Halmashauri nyingine kwa kazi kubwa wanayoifanya sambamba na kuwa na matumizi mazuri ya serikali.


“ Halmashauri ya Kinondoni tangu mwaka 2015 imekuwa ikipata hati safi na hiyo ni kutokana na kuwa na nidhamu ya matumizi mazuri ya fedha za serikali, hati safi inamanisha kwamba mnapokea pesa za serikali lakini pia mnakusanya mapato ya ndani na kuyatumia vizuri” ameongeza.


Kuhusu asilimia 10 ya fedha kwa ajili ya mikopo ya vijana , wakina mama na walemavu,ambayo ni bilioni tatu, Katibu wa ALAT Elirehema Kaaya ameipongeza  Halmashauri kwakufanya vizuri kwani kiasi hicho cha fedha ni sawa na bajeti nzima ya Halmashauri nyingine.


Kaaya amesisistiza kuwa kazi anayoifanya Mkurugenzi  Kagurumjuli ndio inayotakiwa na Rais Dk. John Magufuli na hivyo kuagiza Halmashauri nyingine ziige mfano wake.


“ Umefanya matumizi mazuri na sahihi ya fedha ambazo ni kodi za wananchi wanyonge, kilichofanyika na Mkurugenzi mtedaji wa Kinondoni ni kwamba , Mhe. Rais Magufuli na Waziri wa Tamisemi Suleman Jafo wanasisitiza kutumia local fundi (Force Account) ninashauri wakurugenzi wengine  wasikilize maagizo yanatotolewa na serikali.” Amesisitiza Kaaya.


Awali akizungumza na viongozi wa ALAT, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg Aron Kagurumjuli amesema kuwa Halmashauri imefanikiwa kupata bilioni 32.8 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa miradi mitatu ya kimkakati ambayo itaongeza mapato kwa kiasi kikubwa.


Kagurumjuli alitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa soko la kisasa la Magomeni, wenye thamani ya shilingi bilioni 8.9, ujenzi wa soko la kisasa la Tandale wenye thamani ya shilingi bilioni 8.7 na uboreshaji wa fukwe ya Osterbay (Coco Beach) wenye gharama ya shilingi bilioni 13.


Imeandaliwa na

Kitengo cha Habari na Uhusiano

Manispaa ya Kinondoni

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.