• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya Utumishi
      • Afya na Usafishaji
      • Mipangomiji na Maendeleo ya Makazi
      • Kilimo na Mifugo
      • Elimu Sekondari
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Tehama
    • Kata
      • Kinondoni
      • Magomeni
      • Makumbusho
      • Mwananyamala
      • Kijitonyama
      • Wazo
      • Bunju
      • Mbezi juu
      • Ndugumbi
      • Msasani
      • Kawe
      • Mzimuni
      • Mabwepande
      • Tandale
      • Kigogo
      • Mikocheni
      • Hananasif
      • Kunduchi
      • Makongo
      • Mbweni
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Elimu
    • Afya
    • Maji na Usafishaji
    • Ujasiriamali na utoaji wa mikopo
    • Ushauri katika Kilimo
    • Elimu ya ufugaji mifugo na nyuki
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
  • Madiwani
    • Baraza la madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Vipeperushi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

KINONDONI YAPONGEZWA KUONGOZA MARA NNE MFULULIZO KIMKOA

Posted on: February 24th, 2020

NI KATIKA KUFANYA VIZURI KWENYE MATOKEO YA KIDATO CHA NNE CHA  PILI

 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ,imepongezwa kwa kufanya vizuri katika matokeo ya kidato Cha nne na cha pili kwa miaka minne mfululizo kwa mkoa wa Dar es Salaam.

Pongezi hizo zimetolewa na Afisa Elimu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Hamis Lissu wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa walimu na shule zilizofanya vizuri kwa matokeo hayo kitaifa na kimkoa kwa mwaka 2019 ,2020.

Lissu amesema kuwa Halmashauri hiyo imekuwa ikifanya vizuri na kwa ufanisi mkubwa kwa kila eneo ikiwemo  Elimu, Afya na mazingira, Michezo na maeneo mengine na kusema kuwa mafanikio hayo yanatokana na kuwa na Mkurugenzi mwenye juhudi za kufanya kazi inayoendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Dk. John Pombe Magufuli.

Lissi amefafanua kuwa  Mkoa wa Dar es Salaam unajumla ya Halmashauri tano lakini Halmashauri ya Kinondoni inayo ongozwa na Mkurugenzi wake Aron Kagurumjuli imekuwa ikifanya vizuri katika sekta ya elimu ambapo imeongoza kuwa na matokeo mazuri kwa  miaka minne mfululizo katika mkoa huo.

" Kinondoni imekuwa ikifanya vizuri sana kwenye mambo mengi, binafsi mnanikosha na utendaji wenu uliotukuka ,niwasihi nguvu hii mliyokuwa nayo muendelee nayo ili kuendelea kuwa na rekodi nzuri kwa kuwa mfano bora kwa Halmashauri nyingine zilizopo katika mkoa wetu" amesema Bwana Lissu.

Lakini pongezi hizi pia zimuendee zaidi Mkurugenzi Kagurumjuli, Kinondoni mmepata Mkurugenzi bora, anafanya vizuri sana kwenye Halmashauri yake,na uchapakazi huu ndio anaoutaka Mhe. Rais wetu Dk. Magufuli, tukiwa na wachakazi kama hawa, hakika kwenye mkoa wetu tutakuwa na matokeo makubwa zaidi kwenye kila eneo” ameongeza Bwana Lissu.

Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari, wa Halmashauri hiyo, Bwana Leornad Msigwa  amesema katika matokeo ya kidato cha nne Kinondoni ilishika nafasi ya 39 kati ya Halmashauri 195 na hivyo kufanya kupanda nafasi tatu kitaifa ukilinganisha na mwaka 2018 ambapo ilishika nafasi ya 42 na kuendelea kuongoza kwa kishindo kwa miaka mine mfufulizo katika mkoa wa Dar es Salaam.


Msigwa ameongeza kuwa tathmini ya matokeo ya kidato cha nne  ya mwaka 2019 inaonyesha kuwa ufaulu umeongezeka kwa silimia 0.59 ukilinganisha na mwaka 2018 ambapo ufaulu umekuwa kwa asilimia 81.21 ambapo  mwaka 2019 ufaulu ulikuwa kwa asilimia 81.80.

 Kwa upande wa matokeo ya kidato cha pili , Msigwa ameeleza kuwa  tathmini ya upimaji wa matokeo ya kidato cha pili kwa mwaka 2019 , ufaulu ulikuwa kwa silimia 94.04 na hivyo kufanya Halmashauri ya Kinondoni kushika nafasi ya 24 kitaifa kati ya Halmashauri 184 na hivyo kupanda nafasi 10 kitaifa ukilinganisha na mwaka 2018.

Msigwa amefafanua kuwa, katika matokeo hayo  mwaka 2019 watahiniwa walikuwa 9,340 ambapo waliofaulu mtihani huo kati ya daraja 1-1V walikuwa 8,783 sawa na asilimia 94.04.

Amefafanua kuwa kati yao waliopata alama za ufaulu wa daraja la kwanza ni 1,682,  daraja la piIi ni  1,216, daraja la tatu 1,556, daraja la nne  4,329  huku jumla ya watahiniwa 557 walipata alama ya sifuri.

Katika hatua nyingine Msigwa amewaeleza walimu wa shule za Sekondari waliokuwa katika hafla hiyo kuendelea kujituma zaidi kwa kutumia mbinu mbalimbali za ufundishaji ili kuwezesha Halmashauri hiyo kuendelea kufanya vizuri zaidi kitaifa na kimkoa.

Imetolewa  na Kitengo cha Habari na Uhusiano

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • TANGAZO KUHUSU VIBANDA VYA MWENGE February 22, 2021
  • TAARIFA KUHUSIANA NA WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINA February 18, 2021
  • TANGAZO KUHUSU WAMILIKI WA KUMBI ZA BURUDANI, SHEREHE NA BAA January 22, 2021
  • HAWA HAPA WADAIWA SUGU WA LESENI ZA BIASHARA MANISPAA YA KINONDONI December 04, 2020
  • Tazama zote

Habari mpya

  • WATENDAJI WA KATA NA MITAA KINONDONI TIMIZENI WAJIBU WENU

    April 08, 2021
  • ZIARA YA KATA KWA KATA WILAYA YA KINONDONI YAANZA LEO

    April 01, 2021
  • MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA KINONDONI MHE. SONGORO MNYONGE AKIFAFANUA JAMBO WAKATI WA BARAZA LA MADIWANI

    March 17, 2021
  • UWASILISHWAJI WA TAARIFA ZA KAMATI ZA KUDUMU-BARAZA LA MADIWANI.

    March 17, 2021
  • Tazama zote

Picha Jongefu

DCChongolo akemea vikali wakandarasi wazembe
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ilala Municipal website
  • Ubungo Municipal Council
  • Kigamboni Municipal
  • Temeke Municipal

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • eGoverment Agency
  • Manispaa ya Kinondoni yaongoza katika Makusanyo kufikia Dec.12,2017, 2017.
  • TUME YA UTUMISHI.Tangazo la nafasi za Kazi.

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Dar es salaam, Tanzania

    Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road

    Namba za simu: +255 22 2170173

    Namba ya simu :

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Service

Hatimiliki