Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetakiwa kuanzisha dawati litakalotoa Elimu kwa Mfanyabiashara akiwemo mwenye mtaji mdogo.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ali Hapi alipokuwa kwenye mkutano wa Baraza la Biashara uliofanyika leo katika ukumbi wa Travertine Magomeni jijini Dar es Salaam.
Amesema dawati hilo lilenge hasa mfanyabiashara mwenye mtaji mdogo kujua ni jinsi gani anaweza kuendesha biashara yake na kupata faida.
Aidha amelitaka dawati hilo liwe na uwezo wa kutoa elimu ihusuyo uanzishwaji na uendeshaji wa biashara, jinsi ya kutengeneza faida, jinsi ya kujaza fomu mbalimbali za biashara pamoja na kuwashauri kitaaluma.
Pia amelitaka dawati kuhakikisha linatoa elimu juu ya namna ya kulipa tozo mbalimbali, uwiano kati ya usafi na biashara,pamoja na kuzijua mamlaka mbalimbali zihusianazo na biashara.
Hata hivyo Mh Hapi amewataka wafanyabiashara hao kuhakikisha wanalipa kodi kwa maendeleo ya Wilaya ya Kinondoni na Taifa kwa ujumla.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz