• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya Utumishi
      • Afya na Usafishaji
      • Mipangomiji na Maendeleo ya Makazi
      • Kilimo na Mifugo
      • Elimu Sekondari
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Tehama
    • Kata
      • Kinondoni
      • Magomeni
      • Makumbusho
      • Mwananyamala
      • Kijitonyama
      • Wazo
      • Bunju
      • Mbezi juu
      • Ndugumbi
      • Msasani
      • Kawe
      • Mzimuni
      • Mabwepande
      • Tandale
      • Kigogo
      • Mikocheni
      • Hananasif
      • Kunduchi
      • Makongo
      • Mbweni
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Elimu
    • Afya
    • Maji na Usafishaji
    • Ujasiriamali na utoaji wa mikopo
    • Ushauri katika Kilimo
    • Elimu ya ufugaji mifugo na nyuki
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
  • Madiwani
    • Baraza la madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Vipeperushi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

KINONDONI YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2015-2020, KWA VITENDO

Posted on: June 19th, 2020

Pongezi hizo zimetolewa na Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni kwenye kikao cha majumuisho baada ya ziara ya siku mbili ya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Akizitoa pongezi hizo,  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya kinondoni Ndg Arold Maruma amesema Kinondoni imeonesha uzalendo katika kuhakikisha ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 hadi 2020, inatekelezwa kwa vitendo kwa kutumia makusanyo yao ya Ndani, Fedha kutoka Serikli kuu pamoja na Fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo.

 "Kinondoni kwakweli mmeitendea haki ilani ya uchaguzi ya CCM kwa mwaka 2015-2020, miradi mliotekeleza hapa ni mfano wa kuigwa na mmeacha taswira inayoonekana kwa Wananchi." Ameongeza Mwenyekiti.

Aidha amebainisha kuwa thamani halisi ya fedha imeonekana Katika miradi hiyo kwani mbali na kutumia fedha za ndani, Serikali kuu na wadau, lakini pia  kiasi kilichotumika katika ukamilishaji wake vinaenda sambamba na ubora .

Awali akikabidhi ripoti ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo  kwa Mwenyekiti wa CCM, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesema Kinondoni imeweza kufanikiwa kukamilisha miradi hiyo kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya ofisi yake, Ofisi ya Mkurugenzi na Mstahiki Meya.

Ameongeza kuwa viongozi hawa wa Manispaa na  timu zao wamekuwa  na lengo moja la kuiletea Halmashauri hii maendeleo kwa kuwapatia na kusimamia vyema miradi ambayo inakwenda kumaliza changamoto mbalimbali za Wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndugu Aron Kagurumjuli amesema kuwa Halmashauri imekuwa na utaratibu wa kutenga asilimia 60 ya mapato yake ya ndani na  kuipeleka kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo na asilimia 40 inayobaki kutumika katika matumizi mengine ya kuendesha Halmashauri.

Miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni pamoja na ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri,  Ujenzi wa soko la kisasa la magomeni, Ujenzi wa kituo Cha afya Cha kigogo, Ujenzi wa barabara ya akachube, Ujenzi wa zahanati ya Magomeni, zahanati ya Makumbusho , Ujenzi wa uwanja wa mpira wa kisasa uliopo mwenge na Ujenzi wa stendi ya kisasa ya daladala.

Mingine ni ujenzi wa Kiwanda Cha kuchakata taka na kutengeneza mbolea mboji kilichopo mabwepande,  Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya iliyopo Mabwepande,  Shule ya sekondari ya wasichana ya kidato Cha tano na sita Mabwe Tumaini girls,  Upanuzi wa kituo cha afya Bunju  na Ujenzi wa shule ya Msingi Mkoani.

Imeandaliwa na

Kitengo Cha habari na Uhusiano

Manispaa ya kinondoni.

Matangazo

  • TANGAZO KUHUSU VIBANDA VYA MWENGE February 22, 2021
  • TAARIFA KUHUSIANA NA WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINA February 18, 2021
  • TANGAZO KUHUSU WAMILIKI WA KUMBI ZA BURUDANI, SHEREHE NA BAA January 22, 2021
  • HAWA HAPA WADAIWA SUGU WA LESENI ZA BIASHARA MANISPAA YA KINONDONI December 04, 2020
  • Tazama zote

Habari mpya

  • WATENDAJI WA KATA NA MITAA KINONDONI TIMIZENI WAJIBU WENU

    April 08, 2021
  • ZIARA YA KATA KWA KATA WILAYA YA KINONDONI YAANZA LEO

    April 01, 2021
  • MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA KINONDONI MHE. SONGORO MNYONGE AKIFAFANUA JAMBO WAKATI WA BARAZA LA MADIWANI

    March 17, 2021
  • UWASILISHWAJI WA TAARIFA ZA KAMATI ZA KUDUMU-BARAZA LA MADIWANI.

    March 17, 2021
  • Tazama zote

Picha Jongefu

DCChongolo akemea vikali wakandarasi wazembe
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ilala Municipal website
  • Ubungo Municipal Council
  • Kigamboni Municipal
  • Temeke Municipal

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • eGoverment Agency
  • Manispaa ya Kinondoni yaongoza katika Makusanyo kufikia Dec.12,2017, 2017.
  • TUME YA UTUMISHI.Tangazo la nafasi za Kazi.

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Dar es salaam, Tanzania

    Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road

    Namba za simu: +255 22 2170173

    Namba ya simu :

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Service

Hatimiliki