NI KUFUATIA AGIZO LA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MH PAUL MAKONDA, LA KUHAKIKISHA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ZINAJENGWA MAJENGO YA UTAWALA.
Manispaa ya Kinondoni imeendelea kugawa vifaa vya ujenzi kwa shule 19 kutoka kwa wafadhili ikiwa ni katika kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh Paul Makonda la kuhakikisha shule za Msingi na Sekondari zinajengwa majengo ya utawala.
Vifaa hivyo ni machepe, rato, sururu, majembe pamoja na vyakula ikiwa ni awamu ya Kwanza ya ugawaji.
Zoezi hilo la ugawaji wa vifaa hivyo unaendelea hivi sasa katika shule ya Sekondari Turiani.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz