• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya Utumishi
      • Afya na Usafishaji
      • Mipangomiji na Maendeleo ya Makazi
      • Kilimo na Mifugo
      • Elimu Sekondari
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Tehama
    • Kata
      • Kinondoni
      • Magomeni
      • Makumbusho
      • Mwananyamala
      • Kijitonyama
      • Wazo
      • Bunju
      • Mbezi juu
      • Ndugumbi
      • Msasani
      • Kawe
      • Mzimuni
      • Mabwepande
      • Tandale
      • Kigogo
      • Mikocheni
      • Hananasif
      • Kunduchi
      • Makongo
      • Mbweni
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Elimu
    • Afya
    • Maji na Usafishaji
    • Ujasiriamali na utoaji wa mikopo
    • Ushauri katika Kilimo
    • Elimu ya ufugaji mifugo na nyuki
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
  • Madiwani
    • Baraza la madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Vipeperushi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

KINONDONI KUVITAMBUA, KUVISAJILI NA KUVISIMAMIA VITUO 444 VYA BODABODA NA BAJAJI KATIKA MAENEO YAO

Posted on: November 15th, 2018

Manispaa ya Kinondoni imedhamiria kuboresha chanzo cha mapato kitokanacho na vituo vya bodaboda na bajaji kwa  kuhakikisha  inavitambua, inavisajili na kuvisimamia vituo takribani 444,  vilivyopo katika Kata na Mitaa ya Manispaa hiyo kwa kuzingatia,miongozo sheria, kanuni na taratibu zinazoelekeza kufanya hivyo.

Akitoa muongozo wa zoezi zima la utambuzi huo, katika mkutano wake na madereva wa bodaboda na bajaji uliofanyika katika ukumbi wa King Solomon leo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo amesema,  kwa kushirikiana na wakala wa  barabara za mijini na vijijini TARURA kwa Manispaa ya Kinondoni,  wanatakiwa kuhakikisha suala hilo la utambuzi linafanyika kwa umakini,na wakati,  ikiwa ni pamoja na kusimamia tozo zao zitakazokuwa zikitolewa kwa mujibu wa sheria.

"Manispaa ya Kinondoni, TARURA, itisheni kikao cha Uongozi wa Wilaya, kaeni nao, kubalianeni taratibu nzuri za kuendesha vikundi vyao, vitambueni, visajilini, na mvisimamie tozo zao."Amesisitiza Chongolo.

Awali akitoa taarifa ya vituo hivyo vya bodaboda na bajaji, Mwenyekiti wao ndugu Festo Swai, amesema upo umoja wao uitwao CMPD, ulionzishwa kwa lengo la kusaidiana na kushughulikia changamoto zinazowakabili wao kama vikundi vidogo vidogo, zikiwemo kutosajiliwa na kutambuliwa, kutopatiwa mikopo ya vijana, kutozijua haki zao pindi wanapokutwa na kosa la barabarani, kuuwawa na kuporwa mali zao, pamoja na kupatiwa njia ya kusafirisha abiria mjini.

Akijibu swali linalomtaka bodaboda au bajaji kupelekwa mahabusu pindi afanyapo kosa kwa niaba ya OCD Kinondoni, Inspekta Serengeti amesema, dereva wa bajaji au bodaboda kufanya kazi zake bila kuwa na leseni na viambata vyote atakiwavyo kuwanavyo dereva , atashitakiwa kwa kosa la usalama barabarani.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii anayehusika na Mikopo, Bi Florah Msilu, katika kufafanua suala la mikopo kwa vijana amesema,  kwa mwaka wa fedha 2017/2018, Kinondoni imetenga takribani bilioni 2.7, kwa ajili ya mikopo,  na kuwataka vijana wenye umri kuanzia miaka 18-35,  katika vikundi kuchangamkia fursa hiyo.

Huu ni Mkutano wa kwanza wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kukutana na madereva wa bodaboda na bajaji, pamoja na viongozi wao na  kufanya nao mazungumzo ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero na changamoto walizonazo.

Imeandaliwa na

Kitengo cha Uhusiano na habari.

Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • TANGAZO KUHUSU VIBANDA VYA MWENGE February 22, 2021
  • TAARIFA KUHUSIANA NA WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINA February 18, 2021
  • TANGAZO KUHUSU WAMILIKI WA KUMBI ZA BURUDANI, SHEREHE NA BAA January 22, 2021
  • HAWA HAPA WADAIWA SUGU WA LESENI ZA BIASHARA MANISPAA YA KINONDONI December 04, 2020
  • Tazama zote

Habari mpya

  • WATENDAJI WA KATA NA MITAA KINONDONI TIMIZENI WAJIBU WENU

    April 08, 2021
  • ZIARA YA KATA KWA KATA WILAYA YA KINONDONI YAANZA LEO

    April 01, 2021
  • MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA KINONDONI MHE. SONGORO MNYONGE AKIFAFANUA JAMBO WAKATI WA BARAZA LA MADIWANI

    March 17, 2021
  • UWASILISHWAJI WA TAARIFA ZA KAMATI ZA KUDUMU-BARAZA LA MADIWANI.

    March 17, 2021
  • Tazama zote

Picha Jongefu

DCChongolo akemea vikali wakandarasi wazembe
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ilala Municipal website
  • Ubungo Municipal Council
  • Kigamboni Municipal
  • Temeke Municipal

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • eGoverment Agency
  • Manispaa ya Kinondoni yaongoza katika Makusanyo kufikia Dec.12,2017, 2017.
  • TUME YA UTUMISHI.Tangazo la nafasi za Kazi.

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Dar es salaam, Tanzania

    Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road

    Namba za simu: +255 22 2170173

    Namba ya simu :

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Service

Hatimiliki