• Malalamiko |
    • Anuani zetu |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Municipal Profile
  • Utawala
    • Idara
      • Human Resources
      • AFYA NA USAFISHAJI
      • Urban planning and Land Development
      • KILIMO NA MIFUGO
      • Secondary Education
      • Pre and Primary Education
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Community Development
    • Vitengo
      • sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Tehama
    • Kata
      • Kinondoni
      • Magomeni
      • Makumbusho
      • Mwananyamala
      • Kijitonyama
      • Wazo
      • Bunju
      • Mbezi juu
      • Ndugumbi
      • Msasani
      • Kawe
      • Mzimuni
      • Mabwepande
      • Tandale
      • Kigogo
      • Mikocheni
      • Hananasif
      • Kunduchi
      • Makongo
      • Mbweni
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Education
    • Afya
    • Maji naUsafishaji
    • entrepreneur and Soft Loan
    • Agricultural Consultancy
    • livestock keeping advice
    • Tax collection Centers
  • Madiwani
    • Baraza la madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyomalizika
  • Machapisho
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Miongozo
    • Fomu
    • Taarifa
    • Vipeperushi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
    • Maktaba ya picha jongefu

DC CHONGOLO ASITISHA VIBALI VYA UCHIMBAJI MCHANGA MABONDENI

Posted on: February 4th, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesitisha vibali vya uchimbaji mchanga vilivyotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Ruvu kutokana na kuleta madhara ya uharibifu wa mito na kusababisha athari kwenye makazi ya watu katika Halmashauri hiyo.

Vibali vilivyositishwa katika ni vile vilivyotolewa kufanya shughuli hizo katika Bonde la mto Salasala, Mto mbezi, Ndumbwi, Nyakasangwe, na kusema kuwa mito hiyo inapita katikati ya makazi ya watu na kwamba baada ya kufanyika marekebisho utawekwa utaratibu upya wa kufanya shughuli hizo.

Akizungumza mara baada ya kufanya ziara katika Bonde la mto Salasala (Mto Tegeta) Mhe. Chongolo amesema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya wakandarasi waliopewa vibali hivyo kuharibu mto huo na hivyo kuamuru kupandwa kwa Miti hiyo ambayo itasaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo.

Amesema kuwa kinachofanyika hivi sasa ni kurekebisha mito hiyo kwa kupanda miti, magugu pamoja na mianzi inayoshika ardhi ili kuzuia mmomonyoko wa undongo na hivyo kuweka mkakati wa kuratibu shughuli za utoaji mchanga kufanyika katika maeneo hayo.

Mhe. Chongolo amesena kuwa katika Halmashauri hiyo ameruhusu kibali hicho kutolewa katika bonde la Mpigi kwa maelekezo ya kuhakikisha kuwa shughuli hizo zifanyike kwa ajili ya kusafisha mto ili kuondosha adhari kwani mchanga ukijaa sana husababisha maji kusambaa nje.


“ Wakati tunafanya haya ni lazima tusitishe shughuli zote zinazofanyika hapa, tulifanya tathimini ya kuangalia athari kwa kuunda timu ambayo ilikamilisha majukumu yake na kuleta ripoti hiyo Disemba mwaka jana, mwezi wa kwanza mwaka huu tulianza mjadala na wale ambao walipewa kandarasi ya kutoa mchanga kwenye mito hii” amesema Mhe. Chongolo

Nakuongeza kuwa “ baada ya majadiliano hayo, tulikubaliana nao kupanda Miazi, Miti na Magugu, na watu ambao mnawaona hapa asilimia 90 niliagiza kila mwenye kibali cha bonde anayekuja aje na watu 10 kwa ajili ya kushirikiana kupanda miti, na hii miti inayopandwa hapa sijanunua wameleta wao” ameongeza Mhe. Chongolo.

Mhe. Chongolo amesisitiza kuwa “ kwanza mchanga usiondolewe kibiashara ,tutoe mchanga sehemu ambayo tunaona kuwa kunaongezeko ambalo linaweza kusababisha athari, ili turuhusu maji yapite bila kuleta madhara kwa wananchi waliopo pembezoni mwa mto na huyo anayetoa ahakikishe anafanya marekebisho ikiwemo kupanda miti, magugu na mianzi.


Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amesema kuwa " Tunachangamoto ya watu kufanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya maji, Serikali imeshaelekeza watu ambao wapo kwenye maeneo haya wanatakiwa kuwa umbali wa mita 60 kwa 60 , lakini hatufuati hiyo Sheria ya mazingira.

Wananchi mliopo katika maeneo haya, niwasihi sana acheni kufanya shughuli hapa, leo tunapanda miti ili kunusuru bonde hili lisiendelee kukua, mchanga utatolewa kwa kibali kwa ajili ya kusafisha mto ila sio kuchimba mchanga kwa shughuli ya kibiashara ama nyingine, " amesema Mhe. Chongolo.

Imetolewa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano

 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

Matangazo

  • TANGAZO LA BARAZA LA MADIWANI TAREHE 14/08/2019. August 13, 2019
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI SIKU YA JUMATANO TAREHE 22/05/2019. May 20, 2019
  • TAARIFA KWA UMMA October 16, 2019
  • TANGAZO October 16, 2019
  • Tazama zote

Habari mpya

  • BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAPITISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

    January 07, 2021
  • NI KINONDONI TENA UFAULU WA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2020 MKOA WA DAR ES SALAAM

    December 24, 2020
  • NAIBU WAZIRI-OFISI YA WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA NAMNA KINONDONI INAVYOWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI

    December 22, 2020
  • HOSPITALI YA SANITAS YAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA YA WATUMISHI WAKE

    December 22, 2020
  • Tazama zote

Picha Jongefu

TAMISEMI YAIPOGEZA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ilala Municipal website
  • Ubungo Municipal Council
  • Kigamboni Municipal
  • Temeke Municipal

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • eGoverment Agency
  • Manispaa ya Kinondoni yaongoza katika Makusanyo kufikia Dec.12,2017, 2017.
  • TUME YA UTUMISHI.Tangazo la nafasi za Kazi.

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Anuani zetu

    Dar es salaam, Tanzania

    Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road

    Namba za simu: +255 22 2170173

    Namba ya simu :

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Service

Hatimiliki