• Malalamiko |
    • Anuani zetu |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Municipal Profile
  • Utawala
    • Idara
      • Human Resources
      • AFYA NA USAFISHAJI
      • Urban planning and Land Development
      • KILIMO NA MIFUGO
      • Secondary Education
      • Pre and Primary Education
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Community Development
    • Vitengo
      • sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Tehama
    • Kata
      • Kinondoni
      • Magomeni
      • Makumbusho
      • Mwananyamala
      • Kijitonyama
      • Wazo
      • Bunju
      • Mbezi juu
      • Ndugumbi
      • Msasani
      • Kawe
      • Mzimuni
      • Mabwepande
      • Tandale
      • Kigogo
      • Mikocheni
      • Hananasif
      • Kunduchi
      • Makongo
      • Mbweni
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Education
    • Afya
    • Maji naUsafishaji
    • entrepreneur and Soft Loan
    • Agricultural Consultancy
    • livestock keeping advice
    • Tax collection Centers
  • Madiwani
    • Baraza la madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyomalizika
  • Machapisho
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Miongozo
    • Fomu
    • Taarifa
    • Vipeperushi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
    • Maktaba ya picha jongefu

BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LA PITISHA BAJETI YA BILIONI 170.9

Posted on: January 23rd, 2020

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, katika Mkutano wake maalumu wa Baraza  leo  Alhamisi,  tarehe  23 Januari 2020,   limejadili na  kuidhinisha kwa kauli moja  bajeti yake ya  Tshs  170, 918,524,100/= kwa mwaka wa fedha 2020/2021  ambapo  Tshs.42,951,312, 000/= ni za Mapato ya ndani ya Manispaa na Tshs. 127,967,212,100/= ni Mapato ya Ruzuku kutoka Serikali kuu  zikijumuisha Tshs. 57,018,968,680/= kwa ajili ya  mishahara,Tshs.1,689,501,000/= za matumizi mengineyo na Tshs. 69,258,742,520, /= za  miradi ya maendeleo.

 Kiasi cha ,Tshs. 42,951,312,000/= kilichotengwa na  Manispaa ya Kinondoni kutokana na  makusanyo ya  vyanzo vya ndani vya, Manispaa  kinajumuisha  Tshs.883,467,270/=, kwa ajili ya mishahara ,Tshs. 21,353,714,130,000/= kwa ajili ya matumizi mengineyo na Tshs. 20,714,130,000/= kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

  Azungumza wakati wa kupitisha Bajeti hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh Benjamin Sitta amebainisha kuwa ili kuboresha maisha ya wakazi wa Kinondoni, Manispaa imeandaa mpango wa mwaka 2020/2021 na mpango wa muda wa kati 2020/2021 – 2022/2023 unaolenga kukuza uchumi na kupunguza umaskini na kufikia maendeleo endelevu ya kijamii, kiuchumi,na kimazingira kwa wananchi wake.

Meya Sitta ametanabaisha kuwa Ili kutekeleza dhana nzima ya ugatuaji wa madaraka , mpango huo umeshirikisha jamii katika mpango shirikishi kuanzia ngazi ya Mtaa kwa kuzingatia vipaumbele na  mahitaji halisi ya Wananchi katika maeneo yao na kujielekeza katika kutoa kipaumbele maeneo yanayoweza kutoa matokeo ya haraka yatakayosaidia ukuaji wa uchumi kwa haraka na kwa kipindi kifupi.

Ameyataja maeneo ya kipaumbele kuwa ni pamoja na kuboresha na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kuwekeza katika miradi mikubwa ya Kimkakati, kuboresha miundombinu ya Afya, na Elimu,kuboresha hifadhi ya mazingira na ukusanyaji wa taka, kuimarisha ushirikishaji wa jamii katika upangaji na  utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na uboreshaji wa mazingira ya wafanyabiashara wadogowadogo kwa kuwajengea masoko katika maeneo mbalimbali.

Ili kufikia malengo yaliyokusudiwa,  Mstahiki Meya amewataka viongozi na watendaji wote kusimamia uimarishaji wa mahusiano mazuri kati ya Serikali ,Mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wengine, kujenga uwezo na ujuzi kwa watumishi katika utoaji wa huduma, kuimarisha utawala bora, uwajibikaji na uwazi sambamba na kujenga uwezo kwa viongozi wakiwemo waheshimiwa madiwani na wenyeviti wa Serikali za mitaa katika kusimamia shughuli za Wananchi.

 Aidha Mstahiki Meya   amewashukuru wadau  wote waliofanikisha bajeti hiyo  zikiwemo kamati  zote za kudumu za Manispaa,  Serikali kuu iliyotenga kiasi kikubwa cha fedha kugharamia  Miradi mikubwa ya kimkakati  ya ujenzi wa soko la Tandale, Soko la Magomeni  uboreshaji wa  Fukwe za Cocobeach na miradi mingine ya sekta mbalimbali inayotekelezwa ndani ya Manispaa ya Kinondoni kwa Fedha kutoka Serikali kuu.


Miradi  iliyotengewa fedha kwa Mapato ya  ndani ya Manispaa katika mwaka wa fedha  2020/2021  ni pamoja na ukamilishaji wa kituo cha  kisasa cha daladala Mwenge kwa  milioni 500, ukamilishaji ujenzi wa uwanja wa mpira Mwenge kwa  milioni 500, ujenzi wa standi ya kisasa ya daladala na soko Tegeta nyuki kwa bilioni 3.5, ujenzi wa kituo cha kisasa cha daladala Bunju B  kwa milioni 600,ujenzi wa maabara, famasia, rediolojia, na ununuzi wa gari la kubeba wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya Mabwepande kwa bilioni 1 na ujenzi wa incinerator kubwa kwa ajili ya kuchoma taka za vituo vyote vya kutolea huduma za afya kwa billion 1.5.


Imeandaliwa na

Kitengo cha Habari na Uhusiano

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • TANGAZO LA BARAZA LA MADIWANI TAREHE 14/08/2019. August 13, 2019
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI SIKU YA JUMATANO TAREHE 22/05/2019. May 20, 2019
  • TAARIFA KWA UMMA October 16, 2019
  • TANGAZO October 16, 2019
  • Tazama zote

Habari mpya

  • BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAPITISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

    January 07, 2021
  • NI KINONDONI TENA UFAULU WA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2020 MKOA WA DAR ES SALAAM

    December 24, 2020
  • NAIBU WAZIRI-OFISI YA WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA NAMNA KINONDONI INAVYOWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI

    December 22, 2020
  • HOSPITALI YA SANITAS YAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA YA WATUMISHI WAKE

    December 22, 2020
  • Tazama zote

Picha Jongefu

TAMISEMI YAIPOGEZA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ilala Municipal website
  • Ubungo Municipal Council
  • Kigamboni Municipal
  • Temeke Municipal

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • eGoverment Agency
  • Manispaa ya Kinondoni yaongoza katika Makusanyo kufikia Dec.12,2017, 2017.
  • TUME YA UTUMISHI.Tangazo la nafasi za Kazi.

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Anuani zetu

    Dar es salaam, Tanzania

    Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road

    Namba za simu: +255 22 2170173

    Namba ya simu :

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Service

Hatimiliki